June 7, 2017


Mtoto wa beki wa zamani wa Newcastle, Cheick Tiote ameonyesha kuguswa na msiba wa baba yake licha ya udogo wake.

Rafael ameonekana akiwa na jezi ya Newcastle, mgongoni kukiwa na maandishi ya kumuombea baba yake apumzike kwa amani.

Jezi hiyo imeandikwa mgongoni “RIP Daddy” akionyesha kumuombea baba yake ambaye alianguka baada ya kufariki uwanjani akiwa mazoezini katika timu yake ya Beijing nchini China.

Rafael ana umri wa miaka mitatu na ainaelezwa alikuwa kipenzi cha marehemu Tiote raia wa Ivory Coast.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV