Baada ya bango lililokuwa likielekeza mtaa wa Victor Wanyama kung'olewa, ndivyo hali halisi ilivyo kama unavyoona katika picha.
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Ubungo NHC, Amani Sizya amethibitisha kufutwa kwa Mtaa wa Victor Wanyama.
Sizya amesema watalipeleka suala hilo katika vikao vyao na wanaamini litafanikiwa na utarudishwa na kuwa mtaa wa Wanyama.
Wanyama raia wa Kenya anayekipiga Tottenham, alipewa mtaa ujulikanao kama Viwandani eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ili rasmi uanze kutambulika kama Victor Wanyama.
0 COMMENTS:
Post a Comment