Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Ubungo NHC, Amani Sizya amethibitisha kufutwa kwa Mtaa wa Victor Wanyama.
Wanyama raia wa Kenya anayekipiga Tottenham, alipewa mtaa ujulikanao kama Viwandani eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ili rasmi uanze kutambulika kama Victor Wanyama.
Lakini leo kumeibuka mvutano mkubwa na Sizya amesema kweli walikiuka mambo kadhaa.
“Lakini suala hili tutalipeleka katika vikao vyetu vinavyoihusisha serikali na kulijadili,” alisema.
Sizya aliongeza: “Unajua ilikuwa haraka, lakini niseme ukweli kwamba imani yangu hili litafanikiwa na mtaa huo utatumika kwa jina hilo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment