June 11, 2017
Leo ndiyo ile siku ilikuwa inasubiriwa kwa hamu, fainali ya SportPesa Super Cup.

Ni fainali inayozikutanisha timu mbili za Kenya, AFC Leopards dhidi ya Gor Mahia. Wenyewe wanapenda kusema “Mashemeji Derby”.

Kazi hiyo ni leo, na itakuwa ni mara ya tatu timu hizo zinakutana nje ya Kenya baada ya Gor Mahia kushinda mara zote mbili.

Lakini unaposema Afrika Mashariki, hii ni mara ya kwanza timu hizo zinakutana nje ya Kenya. Si jambo dogo na shabiki wa soka nchini una bahati ya kuipata nafasi hiyo.

Usitegemee kama ndani ya miaka minne hadi mitano ijayo, bahati hiyo inaweza kupatikana tena. Inawezekana itakuwa miaka 10 au 20 ijayo au isitokee kabisa.Sababu kuu ya kwanza ni kwamba unatakiwa kuwa mmoja kati ya wale waliofika uwanjani kuiona mechi hiyo.

Pili unatakiwa kuwa mmoja wale ambao watashuhudia AFC Leopards ikijaribu kushinda mechi yake ya kwanza nje ya Kenya dhidi ya Gor.

Tatu, usisahau, Leopards wanaongozwa na Mtanzania, Denis Kitambi. Kama watashinda na kubeba ubingwa, tayari kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC atakuwa ameweka rekodi mpya.

Nne, mashabiki wa Kenya pale timu zao mbili zinapokutana huwa wanashangiliaje na inakuwaje. Tofauti yao na Watanzania pale zinapokutana Yanga na Simba inakuwaje? Sasa kwa nini usiende kushuhudia mwenyewe na kipute kipo Dar es Salaam?
Tano, vizuri kwenda kujiridhisha. Kwamba mshindi ndiye atarudi Dar es Salaam Juni 13 kucheza na Everton. Je, atakuwa mshindi sahihi, atawaweza Everton. 

Huna sababu ya kukosa eti kwa kuwa hazichezi timu za Tanzania. Soka ni burudani na ndiyo maana unaweza kuchagua kuwa shabiki wa timu ya England au Brazil. Leo, unaweza kuchagua kati ya Gor au Leopards na bado ukainjoy game utakavyo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV