Washambuliaji wameonekana kuwa na thamani kubwa na klabu kubwa zinatenhga kitita kikubwa cha fedha. Maswali imekuwa je, wanastahili. Mimi nimewachangua wafuata na ninaona kuwa wanastahili kununuliwa kwa kiasi hicho. Wewe unaonaje?
ROMELU LUKAKU
THAMANI YAKE: £100m
KLABU ZINAZOMUWANIA: Chelsea
ANASTAHILI? Ndiyo
KWA NINI?
Katika msimu wa 2016-17 ambao umemalizika hive karibuni, Romelu Lukaku raia wa Ubelgiji amefunga mabao 25 kwa klabu ya Everton, hii haijawahi kutokea tokea msimu wa 1985-86 pale gwiji Gary Lineker alipofunga mabao 30.
ALVARO MORATA
THAMANI YAKE: £60m
KLABU ZINAZOMUWANIA: Manchester United
ANASTAHILI? Ndiyo
KWA NINI?
Alvaro Morata amefunga mabao 15, amepiga mashuti 55 katika La Liga. Pamoja na nafasi chache ya kucheza na ushindani mkubwa wa Real madrid lakini yuko kati ya washambulizi 10 Bora wa Hispania.
ANDREA BELOTTI
THAMANI YAKE: £70m
KLABU ZINAZOMUWANIA: Manchester United
ANASTAHILI? Ndiyo
KWA NINI?
Andrea Belotti amefunga mabao 26 katika Serie A msimu uliopita. Mabao hayo, maana yake ni name kuzidizi ya msimu mmoja kabla. Maana yake ni mchezaji ambaye kiwango chake kinazidi kupanda.
ALEXIS SANCHEZ
THAMANI YAKE: £40m
KLABU ZINAZOMUWANIA: Bayern Munich, Chelsea, Manchester City
ANASTAHILI? Ndiyo
KWA NINI?
Imemchukua mechi 101 tu Alexis Sanchez kufikisha mabao 50 katika Ligi Kuu England, si mambo dogo. Amepata nafasi ya tatu ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao 50 kwa kipindi kifupi katika ligi hiyo baada ya magwiji wa Arsenal, Thierry Henry na Ian Wright.
DIEGO COSTA
THAMANI YAKE: £80m
KLABU ZINAZOMUWANIA: Tianjin Quanjian, Atletico Madrid, AC Milan
ANASTAHILI? Ndiyo
KWA NINI?
Diego Costa amefunga ’mabao 20 katika msimu uliopita. Mabao yake yaliisaidia Chelsea kukusanya point 15 zilizoisaidia kuwa bingwa katika Premier League.
0 COMMENTS:
Post a Comment