June 25, 2017
 Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vizuri michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) leo Jumapili kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi A kwenye Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.

Mshambuliaji Ramadhani Shiza Kichuya ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi katika mchezo huo baada ya kuonyesha uwezo wa juu na kufanikiwa kufunga mabao yote ya mchezo huo katika dakika ya 13 na 18.

Ushindi huo umemfanya Kocha Salum Mayanga kuandika ushindi wa tatu katika mechi nne tangu aanze kuifundisha Taifa Stars, Machi, 2017 akichukua nafasi iliyoachwa na Charles Boniface Mkwasa.

Timu nyingine katika Kundi A mbali na Tanzania na Malawi ni Mauritius na Angola wakati Kundi B lina timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe.

Mshindi wa kwanza wa kila kundi atakwenda moja kwa moja hatua ya Robo Fainali. Botswana, Zambia na Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zimefuzu moja kwa moja robo fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV