June 18, 2017


Mashabiki wa michezo na hasa soka wakiongozwa na baadhi ya nyota wa timu ya taifa au waliowahi kuichezea timu ya taifa ya Ivory Coast wamehudhuria mazishi ya kiungo Cheick Tiote.

Tiote alianguka na kupoteza fahamu akiwa mazoezini na timu yake ya Beijing Enterprise nchini China wiki na ushee iliyopita.

Mazishi yake jijini Abidjan uliongozwa na nyota kadha kama Kolo Toure, Wilfried Bony na Salomon Kalou.

Wote hao waliwahi kucheza naye wakati akiwa katika kikosi cha timu ya taifa.


Lakini alianza kutamba nchini Ubelgiji kabla ya kuhamia Uholanzi halafu akajiunga na Newcastle United ya England. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV