June 25, 2017



Uongozi wa Yanga unaamini uko katika wakati mgumu wa mapito lakini mambo yatakaa vizuri.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wanafanya kila juhudi kuhakikisha mambo yanakaa katika msitari.

Hata hivyo, amekiri kwamba hali si nzuri kama ilivyozoeleka.

“Tunapambana sana, kikubwa kinachotakiwa ni kuendelea kushrikiana kwa ukaribu,” alisema.

Mkwasa amesema uongozi wa Yanga unapambana kuhakikisha kila kinachotakiwa kinafanikiwa.

“Watu wanapaswa kuwa wavumilivu na kama nilivyosema tushirikiane,” alisema.


Ingawa uongozi wa Yanga umekuwa ukiendelea kupambana kimyakimya lakini hali halisi inaonekana kifedha hauko vizuri na hata usajili wake umekuwa ukisuasua.

3 COMMENTS:

  1. Kwani lile bakuli la michango ya hiari limeishia wapi?Naomba anayekusanya michango afike nyumbani kwangu nimpatie mchango wangu.

    Hapa ndipo tunapomkubuka Mh.Manji,Mzee akilimali alipambana sana kuhakikisha yanga haimilikiwi na Kampuni ya Manji,kiko wapi sasa,mbona haji kuibeba timu wakati huu ambao timu inahitaji fedha kuliko wakati mwingine wowote?

    ReplyDelete
  2. Wazee wa hizi timu ndo wanaoturudisha nyuma kimaendeleo

    ReplyDelete
  3. Wazee wa hizi timu ndo wanaoturudisha nyuma kimaendeleo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic