Inawezekana Azam FC ikaendelea kuvunjika hasa kwa wachezaji wake waliozoeleka baada ya kuonekana inawezekana hata kiungo Himid Mao, naye akahama.
Himid Mao ameweka wazi kuwa kwa sasa anasikilizia ofa ya timu ya Yanga lakini kama hawatafikia mwafaka klabu hiyo kongwe, ataangalia mipango mingine na hasa nchini Sweden.
Yanga wamekuwa wakiifuatilia kwa ukaribu saini ya Himid kwa ajili ya kumjumuisha ndani ya kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kwa ajili ya kuja kutatua tatizo la kiungo mkabaji ambalo linakisumbua kikosi hicho kwa muda mrefu.
Himid amesema kuwa Yanga ni moja ya timu ambazo wakala wake amekuwa akifanya nazo mazungumzo lakini hata hivyo ana jumla ya ofa saba kutoka timu mbalimbali zikiwemo za Ulaya.
“Mpaka sasa wakala wangu ndiye anazungumza nao Yanga kuhusiana na mimi kujiunga nao, lakini kama hilo litashindikana sitakuwa na wasi sana maana nina ofa za timu saba kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo ile ya Randers ya Denmark ambayo nayo inanihitaji kwa hali ya juu na mazungumzo nao yanaendelea.
“Kuna timu tatu za hapa Afrika lakini kuna timu nne kutoka Ulaya na mimi nitaenda kokote pale ambapo wakala wangu atafanya nao makubaliano kwani siwezi kugoma endapo tu tutakubaliana kunipa vile vitu ambavyo mimi navihitaji,” alisema Himid.
SOURCE: CHAMPIONI
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment