July 13, 2017


Mshambulizi nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu moja kwa moja anaingia katika hesabu za Kocha George Lwandamina.

Lakini atakachotakiwa ni kuhakikisha anafanya kazi ya ziada kujihakikishia namba.

Lwandamina amesema kawaida mchezaji mpya anapoingia kwenye kikosi, anakuwa ni plani mpya ya kocha.

“Lakini nafasi ya kucheza inaanzia na ushawishi kwa mchezaji mwenyewe. Mimi Kocha ningependa wale watakaosaidia timu.

“Kila anayefanya vizuri mazoezini, anakuwa na nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza,” alisema.


Ajibu amejiunga na Yanga akitokea Simba ambayo alianza kuichezea tokea timu ya vijana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV