July 14, 2017Taarifa kutoka Ghana zinasema kwamba basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu kongwe ya Asante Kotoko limepata ajali mbaya.

Timu hiyo ilikuwa inarejea katika mji wake ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo, Kumasi, baada ya mchezo wa ligi kuu mjini Accra dhidi ya Inter Allies FC.

Ajali hiyo imetokea katika sehemu iitwayo Nkawkaw, kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ghana, Accra.


Inasemekana kuwa baadhi ya wachezaji wameumia vibaya akiwemo pia kocha wa timu hiyo na pia kuna kifo cha mtu mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV