July 14, 2017Simba Sports Club 
D'salaam, Tanzania 
13/7/2017. 

         TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 
__________________


Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iiliyokutana jana jioni,kwenye moja ya kumbi za mikutano za Hoteli ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es salaam,imemteua Dr Arnold Kashembe kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu. 

Msomi huyo mwenye shahada ya Uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani Ulaya, uteuzi wake unaanza mara moja. 

Pia kamati hyo imepanga kufanya Mkutano wake mkuu wa kawaida tarehe 13-8-2017, huku pia ikitarajiwa kufanya Mkutano Mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba tarehe 20-8-2017.

Mikutano hyo imeitishwa kwa kuzingatia takwa la kikatiba la klabu,linalotaka notisi ya kuitishwa mikutano hiyo,ifanywe sio chini ya siku Thelathini kabla ya mikutano yenyewe. 

Klabu inatarajia kutoa taarifa zaidi juu ya maandalizi na taratibu za mikutano hiyo katika Siku chache zijazo. 

Mwisho 

klabu inaendelea kuwaomba Wanachama na Washabiki wake muendelee kuwa na utulivu,hususan kipindi hiki ambacho baadhi ya viongozi wetu wakiwa kwenye Shauri lao,liliopo Mahakamani.

Imetolewa na.. 

IDARA YA HABARI YA KLABU YA SIMBA SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV