July 3, 2017Beki wa kati na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amefunguka kuwa kama mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma ameongeza mkataba wa kuitumikia timu hiyo, basi hakuna timu itakayoweza kuwasumbua katika Ligi Kuu Bara msimu ujao, ikiwemo Simba.

Cannavaro ameyasema hayo baada ya Jumatano iliyopita Ngoma kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga. Kabla ya hapo, Ngoma alikuwa amekaribia kutua Simba lakini Yanga wakafanya umafia na kupindua usajili huo wa Msimbazi dakika za mwisho wakati Simba wakiwa wamekubaliana naye kila kitu.

Cannavaro amesema kuwa, limekuwa ni jambo jema kwa upande wao baada ya mshambuliaji huyo kubaki kwenye timu hiyo, hali ambayo itaweza kusaidia kutimiza malengo yao msimu ujao wa ligi kuu.

 “Kiukweli niseme tu kuwa limekuwa ni jambo jema kwa Ngoma kuweza kubaki kwenye timu yetu, nilikuwa nasikia sijui anakwenda Simba kitu ambacho kisingekuwa kizuri upande wetu kama angeondoka kutokana na uwezo alionao, maana timu yoyote inatamani kuwa naye.

 “Unajua ni msimu uliopita tu ndiyo hakuweza kuwa vizuri kutokana na kusumbuliwa na majeraha lakini ukweli kama kweli ndiyo angekuwa ameondoka binafsi ningeumia kwa sababu hakuna beki asiyeujua ubora wake anapokuwa uwanjani, naamini sasa msimu ujao unaweza kuwa vizuri na hasa kwa wapinzani wetu wote watakuwa wamekwisha,” alisema Cannavaro.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV