July 3, 2017




Siku chache tangu uongozi wa Yanga utangaze kumsajili kiungo mkabaji, Papy Kabamba Tshishimbi anayekipiga Mbambane Swallows ya Swaziland, watani wao wa jadi Simba nao wameingia kwenye vita ya kumuwania nyota huyo.

Tshishimbi ambaye ni raia wa DR Congo, Yanga ilimuona wakati Azam FC ilipocheza na Mbabane kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Hata hivyo, kiongozi mmoja wa Simba amesema wala hawana habari na kiungo huyo kwa kuwa Simba imekamilika katika idara hiyo hadi watu hawana nafasi.

"Kweli hizo ni habari mpya kwetu, kiungo ndiyo nyumbani kwa Simba sasa tuanze kuvurugana na watu kwa lipi. Ingekuwa Ngoma sawa naye hatukuwa na haraka naye, tulizungumza naye na tukamuambia wakikubaliana na Yanga asaini. Wakishindwana aje, sasa huyo kiungo hata hatumjui," alisema.

Mcongo huyo ni pendekezo la Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina ambaye ameshinikiza uongozi wa Yanga umsajili katika kuiimarisha safu ya kiungo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba, wameanza kufanya naye mawasiliano kwa njia ya simu kwa ajili ya kumsajili.

Chanzo hicho kilisema, Simba wameanza mipango hiyo ya kumsajili kiungo huyo baada ya kupata taarifa za Yanga kumuwania kwenye usajili wao.

"Tshishimbi ni kati ya viungo bora tunaowahitaji katika kikosi chetu na kikubwa tunamuhitaji kwa ajili ya kumtumia katika michuano ya kimataifa.

"Sisi usajili wetu tunaoufanya hivi sasa kwa ajili ya michuano ya kimataifa na kwa kifupi tunataka kutengeneza kikosi kitakacholeta ushindani katika Kombe la Shiriko Afrika.


"Na ndiyo maana tumeanza mazungumzo na Tshishimbi kwa kufanya naye mawasiliano kwa njia ya simu, hivyo tayari tumeongea naye na tunasubiria ofa yake anayoihitaji," alisema mtoa taarifa huyo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic