July 4, 2017

MADADI

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imewaondoa katika kamati ya uchaguzi wajumbe wanne
 kwenye kamati hiyo.

Uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokaa leo umefanyika baada ya kubaini wajumbe wote wanne walikuwa na matatizo.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi amesema wajumbe wanne walioondolewa, watatu walibainika kukiuka taratibu na kanuni na mmoja aliteuliwa kimakosa.


“Hivyo kamati ya utendaji imeteua wajumbe wote wanne kuziba nafasi zao,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV