July 3, 2017Malinzi na Mwesigwa walifikishwa leo mahakamani Kisutu kwa mara ya pili na kurejeshwa rumande hadi kesi yao watakaporejea kwa mara nyingine Julai 17, mwaka huu.


Wawili hao wanakabiliwa na mashitaka mbalimbali kuanzia 25 hadi 28 likiwemo lile la matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji wa fedha.


Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri  alisema upande wa utetezi wenyewe wanatambua kuwa mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana.

Upande wa utetezi ulikuwa na hoja mbili ambazo ni dhamana na kuharakishwa kwa upelelezi ili kesi isikilizwe.

Lakini upande wa mashitaka ulisisitiza suala la kuzuiwa kwa dhamana.

Mara ya kwanza, Malinzi na Mwesigwa walipandishwa kizimbani Juni 29.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV