July 11, 2017Yule mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda kwa misimu miwili mfululizo, Dany Rusengima ametua kazini kwake.

Rusengimana ametua nchini leo mchana na moja kwa moja kutambulishwa kwa kukabidhiwa jezi ya Singida United.

Singida United wanaodhaminiwa na SportPesa, wameamua kuingia kwa fujo kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kupanda tena msimu ujao.

Myarwanda huyo, anatarajia kutoa ushindani mkubwa katika "kuchana" nyavu kwa msimu ujao na leo ameungana rasmi na kikosi hicho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV