July 5, 2017

Kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr amepata ajira mpya katika kikosi cha Gor Mahia cha Kenya.

Kocha huyo ambaye akiwa Simba alifanya kazi pamoja na Selemani Matola akiwa ni msaidizi wake, amepata shavu hilo na hivyo anaweza kuwemo katika kikosi cha Gor Mahia ambacho kitakuja nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza dhidi ya Everton.


Gor Mahia ilishinda ubingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup hivi karibuni na kupata nafasi ya kucheza katika mchezo huo maalum dhidi ya Everton ya England ambao unatarajiwa kuchezwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV