July 3, 2017

Kipa wa Yanga, Deogratius Munish amegoma kuongeza mkataba na klabu yake ya Yanga kwa kuwa anakwenda kufanya majaribio nje ya nchi.

Kocha wa wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali amesema Dida amewaambia hawezi kusaini, nao wamefikia uamuzi wa kuachana naye.

“Mtu anasema anakwenda kufanya majaribio na hataki kuongeza mkataba. Sasa wewe unataka tufanye nini?

“Tumeona hatuwezi kumsubiri mtu hadi arudi, badala yake tumemsajili yule kipa wa African Lyon, pia tuna Beno Kakolanya.

“Lakini tunaweza kusajili kipa mwingine chipukizi. Basi mambo yataendelea,” alisema Pondamali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV