Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Zimbwe ameanza kupata matibabu nchini Afrika Kusini.
Zimbwe maarufu kama Tshabalala aliumia kifundo cha mguu wa kushoto hali iliyosababisha akae nje kwa zaidi ya wiki mbili.
Beki huyo aliyeibuka kuwa mchezaji bora wa Simba wa msimu uliopita aliumia wakati wa mechi ya Kombe la FA wakati Simba ikiivaa Mbao FC ya Mwanza.
Lakini tayari ameanza kupata matibabu nchini Afrika Kusini.








0 COMMENTS:
Post a Comment