August 7, 2017
Kesi inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange Kaburu imesogezwa mbele hadi Agosti 16, mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Aveva na Kaburu, wamerudishwa tena rumande katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya tano mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambaka. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za klabu hiyo na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya 650 Milioni) na wamekuwa rumande tangu Juni 29 mwaka huu.

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliongozwa na wakili wa mwandamizi wa Serikali, Leonard Chalo na Kishemi Mutalemwa, waliomba wapangiwe tarehe nyingine kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambaka aliliridhia ombi la mawakili wa serikali huku akiwataka kukamilisha upelelezi huo.


 Kufuatia ombi hilo lililotolewa, mawakili wa upande wa utetezi, Philemon Mutakyamirwa na Evodius Mtawala waliiomba mahakama hiyo kesi itajwe tena Agosti 16, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV