August 28, 2017



Baada ya timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza, Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania, ameibuka na kusema kuwa huo ni mwanzo mzuri wa kikosi chake na atahakikisha anauendeleza.

Azam wakiwa ugenini mkoani Mtwara, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya wenyeji wao, Ndanda FC.

Kocha huyo amesema: “Jambo la kushukuru ni kwamba tumeanza vizuri ligi na kushinda pointi tatu tukiwa ugenini, suala hilo linanipa matumaini makubwa ya kwamba tunaweza kufanya vizuri sana kwenye msimu huu.
“Hiki tulichokifanya leo (juzi) nitahakikisha kinaendelea na tunapata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zinazokuja, bila ya kuangalia ni aina gani ya mpinzani ambaye tutakutana naye.”

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic