August 10, 2017


NAHODHA wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard, amemweleza kiungo wa timu hiyo Philippe Coutinho, kama anataka vita basi alamishe kwenda Barcelona.

Barcelona wameshapeleka ofa mara mbili wakimtaka kiungo huyo raia wa Brazil  wakiwa na presha kubwa baada ya Neymar kuondoka hapo na kujiunga na PSG.

Barca wameshaweka wazi kuwa mchezaji anayeweza kuziba pengo la Neymar ni Coutinho tu, hivyo wamekuwa wakipambana sana kuhakikisha wanampata.

“Ni vigumu kumzuia asiondoke, sana sana wachezaji wanaotoka Amerika ya Kusini ambao mara nyingi wamekuwa wakisema kuwa ni ndoto yao kucheza Barcelona.


“Lakini nafikiri Barca wameleta ofa mbili nazo zimekataliwa, nafikiri kama akilazimisha kwenda atakuwa anategeneza vita kwa kuwa Liverpool hawawezi kumuachia kwa urahisi,” alisema Gerrard.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV