August 9, 2017

KIKOSI CHA AZAM FC MSIMU ULIOPITA

Kocha Mkuu wa kikosi cha Azam, Aristica Cioaba raia wa Romania ameweka wazi kuwa makali ya kikosi chake hicho yataongezeka baada ya kurejea nchini wakitokea Uganda ambapo wameenda kuweka kambi.

Azam wamekimbilia nchini Uganda kuweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi utakaoanza Agosti 26, mwaka huu ambapo wakiwa huko watacheza mechi za kirafiki na timu za KCCA, Vipers, URA na Onduparaka.

Mromania huyo amesema kuwa kambi hiyo ya nje ya Tanzania waliyoipata itakiwezesha kikosi chake kujinoa kwa utulivu na kuwasaidia nyota wake kuungana kwa pamoja na kutambuana wanavyocheza, jambo ambalo litasaidia kutimiza kile ambacho anakitaka kwenye msimu ujao.

“Kambi ya huku Uganda ina faida kubwa kwetu, na labda nikuhakikishie kuwa tukitoka huko tutakuwa moto wa kuotea mbali kwenye ligi kuu kwani wachezaji wangu watakuwa wameshika kile nitakachowafundisha kwa kiasi kikubwa.


“Unajua mnapokuwa nje mnapata nafasi ya kuwa huru kufundisha mbinu zako kiutulivu kwa sababu hauna hofu labda watu fulani watakuona kile unachokifundisha, lakini hii ndiyo mara ya kwanza kwa wachezaji wote kuwa sehemu moja, jambo ambalo litafanya wachezaji kujuana kwa urahisi tofauti na muda mwingine tulipokuwa tunajinoa,” alisema Mromania huyo. 

1 COMMENTS:

  1. Safi Azam Jana J4 Wametoka 2-2 na Uganda Cranes(CHAN). Ni pre-season Nzuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic