August 5, 2017
 Mara tu baada ya kutua nchini, beki kisiki wa zamani wa Arsenal, So Campbell tayari amekwenda moja kwa moja kutembelea timu ya walemavu ya Muungano.

Campbell ametua nchini kwa ajili ya ziara ambayo ni mwaliko wa SportPesa Tanzania. Alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa timu hiyo ambao walimwelezea namna ilivyoanzishwa na wanavyoendelea.

Campbell ni katiya mabeki visiki waliowahi kutokea nchini England. Pia ni kati ya mabeki waliocheza kwa mafanikio makubwa katika kikosi cha Arsenal chini ya Kocha Arsene Wenger.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV