August 9, 2017Si vibaya ukusema kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina raia wa Zambia, ameamua kuwakwepa Simba baada ya kusema kuwa hataki kuizungumzia timu hiyo.

Kocha huyo amesema kwa sasa anawaza kuhusu timu yake tu na siyo nyingine yoyote ile iwe kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara au kwingineko.

Mbali na kusema hivyo, pia Lwandamina amewaambia wapinzani wake kuwa msimu ujao atahakikisha anatembeza dozi zaidi ya msimu uliopita ili waendelee kufanya vema kwenye ligi kuu.

"Nafanya kazi kwa Yanga, hivyo kutokana na hilo nimekuwa si mfuatiliaji wa mambo ya timu zingine ikiwemo Simba. Sisi tunaendelea kujiandaa vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri msimu ukianza.


“Nakumbuka msimu uliopita timu zote tulizokutana nazo kwenye ligi zilitusumbua sana, hakuna ambayo ilikuwa rahisi kwetu, lakini kikubwa ambacho naweza kusema ushirikiano ndiyo ulifanikisha tukawa mabingwa, hivyo basi tutahakikisha tunaiendeleza hali hiyo katika msimu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni,” alisema Lwandamina.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Point....unapoiwaza simba tu na kusahau SINGIDA, MTIBWA, KAGERA na nk ujuwe ni mwehu. Kila match kwa wana yanga ni final,,,,tusubilini tunakuja

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV