August 7, 2017

MULAMU

Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mulamu Nghambi, leo Jumatatu amezindua kampeni zake rasmi na kutaja vipaumbele vitano atakayofanyika kazi iwapo atachaguliwa katika nafasi hiyo.

Nghambi ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (Dorefa), anawania nafasi ya makamu wa rais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Katika uzinduzi alioufanya leo, Nghambi ambaye amekuwa kiongozi wa soka kwa miaka 18, alisema kuwa moja ya kitu atakachohakikisha kinakuwa sawa ni suala la ushirikiano na viongozi wengi kwa lengo la kuleta maendeleo ya mchezo huo nchini.

“Endapo nitapa nafasi hii ambayo nawania katika uchaguzi, naahidi kuwa nitaitendea haki kutokana na uzoefu nilionao kwa kutumikia soka katika nyadhifa mbalimbali kwa kipindi cha miaka 18 sasa.


“Dhamira kubwa si kuongelea uzoefu wangu ila kuweka wazi malengo yangu ya msingi yalionisukuma kuwania nafasi hii  ni ushirikiano na viongozi wenzangu, mipango ya muda mfupi, wa wakati na muda mrefu ambayo, naamini itakuwa na faida kubwa katika kukuza soka letu,” alisema Nghambi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic