August 7, 2017


Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa jana imezindua rasmi promosheni ya mtamburishe rafiki ijulikanayo kama Rafiki Bonus ambapo mtamburishaji atajipatia shilingi 2000 kama bonus ya utamburishaji.

Uzinduzi huo, ulifanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo Peninsula House karibu na ufukwe wa Coco, Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas alisema kampuni imekuja na Bonus Rafiki ikiwa kama njia ya kurudisha fadhila kwa wateja wao.

Tarimba alisema, ili mteja afanikiwe kushiriki katika bonus hiyo, mteja anatakiwa awe amejisajili na awe mtumiaji wa SportPesa kubashiri.

"Kampuni yetu imekuja na Bonus Rafiki ikiwa kama njia ya kurudisha fadhila kwa wateja wetu na tunajua wamekuwa wakiwafundisha rafiki zao namba ya ya kubashiri na SportPesa.

"Hivyo, tumeona ni vema na sisi tuwawekee mazingira ya wao kunufaika kwa uaminifu wao na kampuni, Bonus Rafiki inamuwezesha mteja kupata shilingi 2000 kwa kila mteja anayemtaburisha katika jukwaa la kubashiri na SportPesa,"alisema Tarimba.

mwisho

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV