August 14, 2017


Real Madrid imeitwanga Barcelona kwa mabao 3-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kubeba ubingwa wa Kombe la Super Cup la Hispania, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona. Mechi ya pili kwenye Agosti 17 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu itaamua bingwa.

Pamoja na kushinda kwa mabao hayo, nyota wake Cristiano Ronaldo ambaye alifunga bao la pili alilambwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi kusema alijiangusha, akamtwanga kadi ya pili ya njano iliyozaa nyekundu.

Mabao ya Madrid yalipatikana Gerard Pique ambaye amejifunga, Lionel Messi akasawazisha kupitia mkwaju wa penalti lakini Ronaldo akafunga la pili kwa mkwaju mkali nje kidogo ya eneo la 18 baada ya Madrid kufanya counter attack.


Wakati Madrid wakicheza pungufu mtu mmoja baada ya Ronaldo kutolewa katika dakika ya 81, Marco Asensio aliifungia Madrid bao la tatu katika dakika ya 90 na kumaliza mchezo.1. Ter Stegen
3. Piqué
4. Rakitic
5. Sergio
8. Iniesta
9. Suárez
10. Messi
16. Deulofeu
18. Alba
22. Aleix Vidal
23. Umtiti

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV