August 23, 2017



Licha ya kuwa ugenini nchini Ufaransa, Napoli ya Italia imeishinda Nice ya Ufaransa kwa mabao 2-0 katika mechi ya pili ya play-off ya LIgi ya Mabingwa Ulaya.

Ushindi huo unaifanya Napoli kuingia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-0 na kuicha Nice ikibaki nyumbani na hasira za mashabiki wake zikimalizikia kwa mshambuliaji wao Mario Balotelli.

Mashabiki hao waliamua kumzomea Balotelli wakati wa mchezo huo wakiamini hakuwa makini. Balotelli alikuwa akimlaumu mwamuzi kutokana na bao moja la Napoli.

Kutokana na mashabiki kumzomea mfululizo, kocha wake alilazimika kumtoa nje na kumuingiza Ganago katika dakika ya 77.

VIKOSI VILIVYOKUWA:
Nice: Cardinale, Souquet, Le Marchand, Dante, Jallet, Tameze (Lees-Melou 66), Seri, Walter (Marcel 79), Sneijder, Balotelli (Ganago 77), Saint-Maximin. 
Subs not used: Benitez, Srarfi, Burner, Sarr.
Booked: Seri, Lees-Melou


Napoli: Reina, Hysaj, Albiol, Koulibaly, Ghoulam, Allan (Rog 71), Jorginho (Diawara 85), Hamsik (Zielinski 63), Callejon, Mertens, Insigne. 
Subs not used: Sepe, Maggio, Chiriches, Milik.
Booked: Koulibaly
Goals: Callejon 48, Insigne 89 
Referee: Damir Skomina (Slovenia)






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic