August 23, 2017



Winga wa Yanga, Geofrey Mwashiuya, ameamua kuanza mapema mazoezi ya gym ili kujiweka fiti zaidi aweze kumshawishi kwa haraka kocha wake, George Lwandamina katika kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mwashiuya ambaye kwa muda mrefu yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu, mtayari ameanza mazoezi hayo katika Gym ya London iliyopo Kinondoni jijini Dar na leo atakuwa jukwaani Yanga ikiivaa Simba kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, Mwashiuya anaendelea vizuri na anafuata ratiba ya mazoezi aliyopewa.

Kwa upande wake, Mwashiuya amesema: "Naendelea vizuri, naamini siku si nyingi nitakuwa fiti kama zamani na kuanza kuitumikia timu yangu.


"Nimepewa programu ya mazoezi niwe nafanya ili kurudi katika hali yangu ya kawaida na nimekuwa nikifanya hivyo kila siku, nataka niwe fiti kabisa ili kocha Lwandamina aweze kunipa nafasi ya kucheza kwani nafahamu kama nisipokuwa fiti nitaishia kukaa nje tu."

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic