September 15, 2017


Hizi timu zinapendwa asee, pamoja na mapokezi ya “kufa mtu” waliyoyapata Yanga wakati wakitua mjini Songea, basi lao limegeuka dili.

Yanga iko mjini Songea kuivaa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini humo, kesho.

Lakini mashabiki, wamekuwa wakijazana nje kwa wingi katika hoteli waliyofikia Yanga wakipiga picha.

Baadhi ya wapigapicha wa kulipisha, bao wamejitokeza eneo hilo na wamekuwa wakiwapiga picha watu na kwenda kusafisha haraka ili kujipatia kipato.


Baadhi ya mashabiki, wao wamekuwa wakipiga picha wakiwa katika basi hilo kwa kutumia simu zao za mkononi lakini ikiwa ni sehemu ya kutimiza furaha yao ya kuwa karibu na basi la mabingwa hao wa Tanzania Bara.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic