September 15, 2017



Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji ya Songea.

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea kujiandaa na mechi hiyo ya kesho.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kukishuhudia kikosi cha Yanga ingawa kulikuwa na tafrani kabla ya timu hiyo kuingia uwanjani.

Yanga wametua mjini Songea jana, lakini walikosa sehemu ya mazoezi hivyo kulazimika kupumzika.

Katika mazoezi ya leo, Yanga walipasha misuli, baadaye wakawa wanaruka koni kabla ya kuanza mazoezi ya kawaida kama mechi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic