September 18, 2017


Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ametua katika mahakama ya Kisutu na kupata nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wake wa zamani, Yusuf Manji.


Manji ni mwenyekiti wa Yanga mstaafui baada ya kuamua kuachia ngazi miezi michache iliyopita.

Manji alikuwa mahakamani hapo akikabiriwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya.

Kesi hiyo inayomkabiri Manji kuhusiana na kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika mahakama ya Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.

Suala la kushindwa kusikilizwa ,limetokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani, lakini naye alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu yuko katika kikao.

Kutokana na hali hiyo, imesogezwa mbele hadi Septemba 25, Manji atakapotakiwa kuleta mashahidi wake.


Manji anatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic