September 18, 2017



Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji kuhusiana na kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika mahakama ya Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.

Suala la kushindwa kusikilizwa ,limetokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani, lakini naye alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu yuko katika kikao.

Kutokana na hali hiyo, imesogezwa mbele hadi Septemba 25, Manji atakapotakiwa kuleta mashahidi wake.


Manji anatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic