September 7, 2017



Hali ya beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe inaonekana kumridhisha daktari wa timu hiyo na sasa amempangia kuanza mazoezi Jumatatu ijayo.

Kapombe ataanza mazoezi Jumatatu baada ya zile wiki mbili za nyongeza kwisha.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mazoezi ya Kapombe yatakuwa ya taratibu.

"Ataanza mazoezi taratibu kwa kuwa ndiyo anarejea katika mazoezi," alisema.

Kapombe amekuwa akisumbuliwa na nyonga, jambo ambalo Simba waliamua kulifanyia kazi kwa kina kuhakikisha anakuwa katika hali yake.

Beki huyo amerejea Simba ambayo aliondoka na kwenda kujiunga na Azam FC kabla ya kwenda nchini Ufaransa ambako alijiunga na AS Cannes, hata hivyo, hakudumu sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic