September 7, 2017



Wakati kipa wa Simba, Said Mohamed anaondoka siku chache zijazo kwenda India kwa matibabu, atakaporejea atalazimika kukaa wiki sita nje ya uwanja kabla ya kuanza matibabu.

Mohammed maarufu kama Nduda aliumia hivi karibuni na Simba ikaamua kumpatia matibabu sahihi.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wako katika hatua ya mwisho kupata visa.

"Baada ya kupatikana kwa visa, safari itaanza kama ilivyopangwa. Lakini akirejea ndiyo hivyo atapumzika kwanza," alisema.

Nduda amejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ikiwa ni siku chache baada ya kucheza mechi moja ya michuano ya Cosafa na kuibuka kipa bora wa michuano hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic