September 18, 2017




Kesi namba 214  nayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva nA Makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' imetajwa tena kwenye mahakama ya hakimu mkazi kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victori Nongwa.

Katika kesi hiyo ambayo leo iliitwa kwa ajili ya kitajwa ambapo upande wa uendesha mashitaka uliowakilishwa na wakili wa serikali Nassor Katuga akisaidiwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 'Takukuru', Peter Vitalis.

Katuga ameimbia mahakama hiyo kuwa tayari wameshakamilisha upepelezi wa kesi hiyo na wamepeleka jarada kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP), kwa ajili ya kupitia upelelezi huo ili kuona kama umekamilika kabla ya hatua nyengine kuendelea.


Kutokana na hivyo, hakimu Victoria Nongwa ameharishia kesi hiyo hadi Septamba 27,  mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo baada ya kueleza upande wa utetezi uliowakilishwa na wakili, Philemon Mutakyemirwa akisaidiwa na Evodious Mtawala.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic