September 26, 2017


Kesi inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji imeendelea kuunguruma leo jijini Dar es Salaam.


Kesi hiyo ya tuhuma ya madawa ya kulevya imeendelea leo katika Mahakama ya Kisutu, Manji na mashahidi wa upande wa utetezi, wakitoa utetezi wao.

Kesi hiyo katika suala la kutoa ushahidi upande wa mshitakiwa ulianza jana na itaendelea kwa siku tatu, yaani leo, kesho na keshokutwa.

Manji ameanza kujitetea hiyo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu kesi yake ya dawa za kulevya inayomkabili.

Kesi hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa upande wa ushahidi kuanza kutoa utetezi wao ambao leo imekuwa ni siku ya kwanza  kwa mashahidi watatu akiwemo Manji mwenyewe.

 Licha ya mwenyekiti hiyo wa zamani wa Yanga na diwani wa kata ya Mabagala KUU  kutoa utetezi wake wengine walikuwa Daktari wa Hospital ya Aga Khan, Profesa Mustapha Bapumia na bingwa wa magonjwa wa Toto, DR Khan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic