September 6, 2017


Na Khadija Mngwai
KIUNGO Mshambuliaji wa Difaa El-Jadida, Simon Msuva, ameibuka na kusema kuwa kwa namba aliyopangwa sasa na kocha wake katika klabu yake hiyo mpya, anatarajia kutupia mabao mengi na kutwaa ufungaji bora.

Msuva alifanikiwa kuifungia Stars mabao mawili kwenye ushindi wa 2-0, katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana wikiendi iliyopita, katika Uwanja wa Uhuru huku akionyesha kiwango cha hali ya juu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Msuva alisema, anahitaji kuendeleza kasi ya kuzifumania nyavu katika timu yake hiyo mpya kwa kuwa lengo lake ni kuona anafika mbali zaidi na kitendo cha kupangwa namba kumi badala ya pembeni alipokuwa, anaona kuwa kinamsaidia kuwa bora.

“Namba ambayo nimebadilishwa kwa sasa itanisaidia kuweza kuzifumania nyavu zaidi na kuwa bora katika timu yangu, lengo langu kubwa si kuishia hapa nilipo kwani nahitaji kusonga mbele zaidi kwa kwenda Hispania ama sehemu yoyote ile, hivyo kwa sasa kuna mikakati nimeipanga kuona naweza kufanikiwa.

“Bado nina malengo nimeyapanga naamini Mungu atanisaidia, hivyo namba ambayo nimebadilishwa nina imani nayo ya kuweza kufanya vizuri na nitamuonyesha uaminifu mwalimu kama alivyonionyesha yeye kuhakikisha nazifumania nyavu ikiwezekana kutwaa ufungaji bora wa Morocco ili niwe na uhakika wa kwenda mahali kwingine,” alisema Msuva.

“Kuhusu suala la mimi kutumia biblia ni jambo la kawaida kwani nimekuwa nikitumia tangu nilivyokuwa mdogo na familia yangu imeokoka hivyo ni kitu ambacho kimenijenga sana, mara nyngi huwa nakaa nayo kambini na kuisoma pale ambapo naona majukumu ya kitimu hayapo,” alisema Msuva.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic