September 24, 2017


Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kumkosa Papy Tshishimbi katika mechi ijayo ni pengo lakini wako watakaoziba pengo lake.

Nsajigwa amesema benchi la ufundi litaanza kulifanyia kazi mapema pengo hilo watakapokutana na Mtibwa Sugar, Jumamosi ijayo.

“Lazima tulifanyie kazi na tuna muda, hivyo litakuwa pengo ambalo tutaliziba,” alisema.

Tshishimbi raia wa DR Congo ambaye ni kiungo mpya wa Yanga, ameweka rekodi ya kupigwa kadi tatu za njano ndani ya mechi nne.


Kadi yake ya tatu alipigwa jana katika mechi dhidi ya Ndanda FC, mechi ambayo Yanga ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic