September 24, 2017




Baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC, Simba imesafiri hadi mjini Tabora ambako inaendelea na maandalizi ya mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.

Simba iko mjini Tabora na leo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wake Milambo FC.

Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Simba, amesema mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ijayo.


“Mechi ya kirafiki na Milambo ni leo, baada ya hapo tutaendelea na maandalizi mengine. Tutarejea kambini kumalizia maandalizi kabla ya kuwavaa Stand,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic