September 13, 2017


Kocha Joseph Omog anaendelea vizuri baada ya ile ajali ya kugongana na mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi wakiwa mazoezini.

Okwi naye imeelezwa kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata ‘ajali’ kwa kugongana na kocha wake kwenye mazoezi ya Uwanja wa Uhuru.

Hata hivyo, mmoja wa maofisa wa Simba amesema, Omog alikuwa akisikia maumivu ya kichwa hata baada ya mazoezi.

"Tuna imani ataamka vizuri kesho. Waligongana kwa nguvu kwa kweli. Ilikuwa ni bahati mbaya na wote tumeona, hivyo tunawaombea wawe vizuri,"alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic