September 15, 2017


Mashabiki wa Yanga na wengine wa soka walilazimika kubaki nje baada askari kuwazuia kuingia ndani kushuhudia mazoezi ya kikosi cha Yanga.

Yanga ipo mjini Songea kusubiri kuivaa Majimaji ambayo imeweka kambi nje ya mji wa Songea katika eneo la Peramiho.

Wakati Yanga ikiendelea na mazoezi, mashabiki wa Yanga walijazana nje ya uwanja wa Majimaji wakitaka kuingia ndani lakini juhudi zao zilikwama.

Askari walifanya hivyo baada ya kuanza kwa tafrani kati ya mashabiki wa Yanga na Majimaji, hali iliyosababisha ulinzi kuimarishwa.

Tayari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy ametangaza kutakuwa na ulinzi mkali katika mechi ya Ligi Kuu Bara wakati Majimaji watakapoivaa Yanga kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic