September 6, 2017


Safari ya kipa wa Simba, Said Mohammed ‘Nduda’ kwenda nchini India kwa matibabu ya mguu inatarajiwa kuwa wikiendi hii inayokuja.

Taarifa kutoka Simba zinaeleza kuwa maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na kilichobaki ni mchezaji huyo tu kuondoka nchini.

Kipa huyo bora wa michuano ya COSAFA 2017 iliyofanyika nchini Afrika Kusini, alisajiliwa hivi karibuni akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Ikumbukwe kuwa aliumia wakati alipokuwa katika kambi ya Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya, Yanga, mchezo uliochezwa Agosti 23, mwaka huu. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic