September 20, 2017



Ikiwa ndiyo kwenda katika mchezo wa kesho Alhamisi kati ya wenyeji Mbao FC na Simba, benchi la ufundi la Simba limesema kuwa, wapinzani wao hao siyo wa kuwachukulia poa.

Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, imeyasema hayo na kubainisha kuwa, msimu uliopita, walipata shida sana kuondoka na ushindi walipokutana na timu hiyo hasa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambao watachezea keshokutwa.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema Mbao ni miongoni mwa timu imara hasa zinapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, hivyo wamejipanga kikamilifu kukabiliana nao.

“Nakumbuka msimu uliopita tulipoenda kucheza mechi ya ligi kwao, ilituwia vigumu sana kuondoka na alama tatu kwani hadi dakika ya 80, tulikuwa nyuma kwa mabao 2-0. Tukapambana zaidi tukaibuka na ushindi wa mabao 3-2.


“Lakini hata kwenye fainali ya Kombe la FA, licha ya kushinda kwa mabao 2-1, lakini walitupa wakati mgumu, hivyo tunaenda kupambana nao tukiwa kamili lengo ni kuhakikisha tunapata pointi tatu na kukaa kileleni,” alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic