September 20, 2017




Yanga wanatarajia kurejea mazoezini leo kwenye Uwanja wa Uhuru ikiwa ni siku moja badaa ya wachezaji kugoma, jana.

Wachezaji waligoma kufanya mazoezi kwenye uwanja huo jana wakitaka kulipwa malimbikizo ya mshahara wa miezi miwili.
Lakini taarifa zilizoifikia SALEHJEMBE, zimeeleza, viongozi wa Yanga watakwenda mazoezini leo kuzungumza na wachezaji.
“Viongozi watakwenda mazoezini, lengo ni kuzungumza na kuwaahidi wachezaji ili waanze mazoezi na wao walimalize suala lao hilo,” kilieleza chanzo..


Baadhi ya wachezaji wa Yanga, jana walionekana katika sehemu mbalimbali za Uswahilini wakipasha misuli ili kujiweka vizuri kwani pamoja na kugoma wanajua wana majukumu ya Ligi Kuu Bara mbele yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic