September 14, 2017


Kikosi cha Yanga kimetua salama mjini Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mechi yao dhidi ya Majimaji maarufu kama Wana Lizombe.

Yanga itafanya maandalizi dhidi ya Majimaji ambayo watashuka dimbani keshokutwa Jumamosi kuivaa katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Kwa Yanga itakuwa ni mechi ya tatu msimu huu, ikiwa ya pili ikiwa ugenini baada ya kucheza mechi moja nyumbani na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Lipuli FC kabla ya kuivaa Njombe ikiwa nyumbani na kuichapa 1-0.
Awali Yanga, walisema watafanya mazoezi leo lakini kumekuwa na taarifa wameamua kupumzika hadi hapo kesho watakapoanza maandalizi ya mechi hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic