September 14, 2017


Mazeozi ya Simba yameendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na inaonyesha kuwa wachezaji wako makini na wanataka kuwa fiti hasa.

Hiyo inatokana na mazoezi makali ambayo yalifanyika kwenye uwanja huo na wachezaji kuchuana vikali utafikiri ni mechi.

Wachezaji wa Simba walianza kuchuana katika mazoezi ya kasi hasa kukimbia na baadaye wakapiga katika mchezo wa ushindani kila mmoja akitaka kushinda dhidi ya mwenzake.


Simba inajiandaa na mechi dhidi ya Mwadui FC ambayo itakuwa ni mechi yake ya tatu ya Ligi Kuu Bara baada ya kuanza na ushindi wa kishindo wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na baadaye wakapata sare ya 0-0 dhidi ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic