September 7, 2017

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam alfajiri ya Ijumaa kuelekea Njombe kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Njombe Mji utakaochezwa keshokutwa Jumapili.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utapigwa kwenye Uwanja wa Saba Saba ikiwa ni mwendelezo wa ligi hiyo msimu wa 2017/18.

Wachezaji wa Yanga ambao wanatarajiwa kuachwa katika safari hiyo ni kipa Beno Kakolanya, kiungo Geoffrey Mwashiuya na washambuliaji Mzambia Obrey Chirwa na Amissi Tambwe kutokana na kuwa majeruhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic